Thursday, June 12, 2008

Monday, May 19, 2008

CAST PLANT

Huu ni mmea ambao umezoeleka kuonekana maeneo mengi ya Tanzania, mme huu hutoa mbegu ambazo zinatoa mafuta (cast oil) kiasi cha 40% - 60%. Mafuta haya yanakuwa na kemikali ya recin ambayo ni sumu.


Sumu iliyomo kwenye mbegu za mimea hii inauwezo wa kuua binadamu kwa kiasi kidogo chambegu 2 - 3 kwa mtoto mdogo ma mbegu 8 kwa mtu mzima
MATUMIZI
Mafuta haya yanauwezo mkubwa wa kutibu fangasi za miguu, maonjwa ya ngozi na miguu kupasuka, pia yanasaidia kufunga choo kwa wale wenye tatizo hili lakini yanywewe katika kiwango kidogo sana kwa sababu ni sumu

Saturday, May 03, 2008

KOBE-TORTOISE


Huyu ni kiumbe rahisi sana kumfuga kwa sababu joto la mwili wake linarekebishika kutegemeana na mazingira (ectothemic)

MAZINGIRA
Unaweza kumfuga ndani ya nyumba, lakini ni vizuri sana kama utamweka mazingira nje. Mazingira yawe makavu na upande mwingine kuwe na bwawa dogo la maji, haya maji ni ya kunywa na wale kobemaji hupenda kuogelea humo. Hakikisha wapo katika mazingira masafi kwa sababu wanauwezo wa kubeba vijidudu vya magonjwa yanayodhuru binadamu.

CHAKULA
Ukimfuga katika mazingira asili ya nje ataweza kujitafutia chakula chake na wewe utamwongezea kidogo tu cha ziada
(concentrates)
Kobe kwa kawaida hula majani na mboga mboga, uyoga, wadudu na minyoo. Pia unaweza kuwapa chakula cha mbwa (kidogo) kama chakula cha ziada.

KUKU-(gallus gallus)


Friday, April 25, 2008

Saturday, January 05, 2008

MKARATUSI NA UKWAJU (eucalyptus & tamarind) TIBA YA KIFUA




Mikaratusi na ukwaju ni tiba yenye nguvu dhidi ya kifua na kukohoa, tiba hii ni rahisi kuandaa na haina gharama.
UAANDAAJI
Chukua jani moja au zaidi ya mkaratusi lililokomaa kotoka katika matawi machanga/mapya ya mti, ponda ponda na uchuje kwenye maji kiasi cha mililita 100-200, unaweza kutumia blender pia kusagia dawa hii, kisha changanya na juisi ya ukwaju, pia unaweza kuongezea tangawizi kidogo ukipenda.
MATUMIZI
Kunywa mchanganyiko huu mara 3 kwa siku kwa siku 3-5
Ukitumia mchanganyiko huu mara moja kwa wiki ni kinga tosha kwa magonjwa ya njia ya hewa
NB Ukichemsha majani ya mkaratusi chumbani na kacha mvuke usambae chumbani ni kinga tosha juu ya mafua, pia huleta harufu nzuri chumbani (air freshener)

Friday, January 04, 2008

MBAAZI KAMA DAWA-cajanus cajan









Mbaazi ni zao la chakula ambalo linalimwa sehemu nyingi sana hapa nchini, zao hili pia linaweza kutumika kama dawa kwa kutumia majani, mizizi na maua


MAANDALIZI

Chukua majani, maua au mizizi kiasi cha nusu kilo (ni vizuri kama utachanganya vyote) pondaponda na uloweke kwenye maji safi kiasi cha lita 2 kwa muda wa masaa 24.


Chuja na uweke dawa hii mbali na jua/joto, ni vizuri kama ataweka kwenye friji, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 kwa siku 3


TIBA

Dawa hii inaweza kutibu magonjwa yafuatayo

1-Inauwezo mkubwa wa kushusha homa

2-Husaidia kuponesha vidonda.

3-Husaidia kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake.

4-Husaidia kupunguza uvimbe

5-Huponyesha kifua na kukohoa.

6-Husafisha kibofu/njia ya mkojo.

7- Huongeza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbali mbali

Monday, December 24, 2007

TEAK-MITIKI (tectona grandis)


Hii ni moja ya miti inayotoa mbao aghali zaidi duniani, hii ni kwa sababu mbao hii haiharibiwi kirahisi na maji kwa sababu ina mafuta yanayoteleza, pia huwa haiathiriwi na mchwa

MBEGU
Mbegu za mitiki huloekwa kwa siku 3-4 katika maji yatembeayo, au katika vyombo na kubadilishwa maji kila baada ya ya masaa 12. kabla ya kuloekwa onaziweka kwenye gunia na kufunga na kitu kizito kama jiwe ili kuzizamisha chini. Baada ya hapo unazianika mpaka zikauke vizuri




KITALU
Mbegu zipandwe kwa msitari na nafasi kati ya msitari na msitani ni sentimeta 10 na zifukiwe chini kina cha sentimeta 1. Kitalu kiwe na mwanga wa kutosha kwa sababu kwenye kivuli mbegu hazitaota na zimwagiwe maji kila siku, kilo moja ina wastani wa mbegu 1500 na uotaji ni asilimia 40-60. Mbegu zitaanza kuota baada ya wiki 4-7 na kipindi chote zinahitaji maji ya kutosha na udongo uwe hautuamishi maji.

UPANDAJI
miti hii hupandwa mara baada ya mvua ya kwanza kuanza, unaweza kutumia vipandikizi, miche au hata matawi. Kipimo ni umbali wa mita 2.5-3 kati ya mche na mche, ekari moja inatosha miche 504. miti inayongolewa kwenye kitalu inakatwa mzizi na shina na kubakia shina 25% na mzizi 75% hii husaidia kuzuia upotevu wa maji na kupata mti ulionyooka utakapoota upya.

UVUNAJI
Uvunaji wa kwanza huanza baada ya miaka 6-8 ambapo uaweza kuvuna nusu ya miti kama nguzo za kujengea, hii hufanyika ili kuipa nafasi miti inayobaki kukua zaidi.
Uvunaji wa pili ni baada ya miaka 12-15 ikifuatiwa na 20 kisha 25, katika hivi vipindi ndipo utakapopata mbao na kadri mti unavyochelewa kuvunwa ndio ukubwa na thamani ya mbao inaongezeka

LEUCAENA-VIBIRITI








Hii ni aina ya miti yenye matumizi mengi ambayo unaweza kuikuta katika miti midogo mingi pamoja kama kichaka mpaka miti mikubwa kabisa ya kutoa mbao

MATUMIZI
1-Hutumika kama chakula cha mifugo na ina protein kiasi cha 3-5% pia ina nitrogen ya kutosha kwa wanyama wenye matumbo manne (ruminants) kwa wanyama wenye tumbo moja (non ruminants) kama farasi, punda na nguruwe isitumike zaidi ya nusu ya mlo kwa sababu ina sumu inayojulikana kama mimosine ambayo inasababisha kunyonyoka manyoya

2-Pia hutumika katika kuongeza mbolea kwenye udongo kwa kiasi cha N 2-45%, P 0.2-0.4%, K1.3-4%, Ca0.8-2% na Mg 0.4-1%, hupandwa kwenye shamba linalopumzishwa au kuchanganywa na mazao ili kurutubisha ardhi.

3-Kwenye maeneo yaliyoathirika na ukataji wa miti, leucaena hutumika katika kurudisha uoto. Hii ni kwasababu inakua haraka sana na inasambaa kama moto nyikani, inaweza kupandwa kwa kumwaga mbegu na zikaachwa kuota zenyewe au kwa kupanda miche. Kama kuna sehemu unataka ijae miti haraka panda miti hii hata kama ni michache itasambaa yenyewe, ingawa kwenye sehemu zenye baridi inakua kwa tabu kidogo.

4-Mbegu zake zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa kama bisi, hii hufanyika mara nyingi wakati wa uhaba wa chakula kwa sababu ukusanyaji wa mbugu unasumbua kidogo

5-Matumizi mengine ni mbao, kuni na fito za kujengea, miti hii hutoa mbao nyekundu ambazo zinaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali.