Monday, December 24, 2007

TEAK-MITIKI (tectona grandis)


Hii ni moja ya miti inayotoa mbao aghali zaidi duniani, hii ni kwa sababu mbao hii haiharibiwi kirahisi na maji kwa sababu ina mafuta yanayoteleza, pia huwa haiathiriwi na mchwa

MBEGU
Mbegu za mitiki huloekwa kwa siku 3-4 katika maji yatembeayo, au katika vyombo na kubadilishwa maji kila baada ya ya masaa 12. kabla ya kuloekwa onaziweka kwenye gunia na kufunga na kitu kizito kama jiwe ili kuzizamisha chini. Baada ya hapo unazianika mpaka zikauke vizuri




KITALU
Mbegu zipandwe kwa msitari na nafasi kati ya msitari na msitani ni sentimeta 10 na zifukiwe chini kina cha sentimeta 1. Kitalu kiwe na mwanga wa kutosha kwa sababu kwenye kivuli mbegu hazitaota na zimwagiwe maji kila siku, kilo moja ina wastani wa mbegu 1500 na uotaji ni asilimia 40-60. Mbegu zitaanza kuota baada ya wiki 4-7 na kipindi chote zinahitaji maji ya kutosha na udongo uwe hautuamishi maji.

UPANDAJI
miti hii hupandwa mara baada ya mvua ya kwanza kuanza, unaweza kutumia vipandikizi, miche au hata matawi. Kipimo ni umbali wa mita 2.5-3 kati ya mche na mche, ekari moja inatosha miche 504. miti inayongolewa kwenye kitalu inakatwa mzizi na shina na kubakia shina 25% na mzizi 75% hii husaidia kuzuia upotevu wa maji na kupata mti ulionyooka utakapoota upya.

UVUNAJI
Uvunaji wa kwanza huanza baada ya miaka 6-8 ambapo uaweza kuvuna nusu ya miti kama nguzo za kujengea, hii hufanyika ili kuipa nafasi miti inayobaki kukua zaidi.
Uvunaji wa pili ni baada ya miaka 12-15 ikifuatiwa na 20 kisha 25, katika hivi vipindi ndipo utakapopata mbao na kadri mti unavyochelewa kuvunwa ndio ukubwa na thamani ya mbao inaongezeka

LEUCAENA-VIBIRITI








Hii ni aina ya miti yenye matumizi mengi ambayo unaweza kuikuta katika miti midogo mingi pamoja kama kichaka mpaka miti mikubwa kabisa ya kutoa mbao

MATUMIZI
1-Hutumika kama chakula cha mifugo na ina protein kiasi cha 3-5% pia ina nitrogen ya kutosha kwa wanyama wenye matumbo manne (ruminants) kwa wanyama wenye tumbo moja (non ruminants) kama farasi, punda na nguruwe isitumike zaidi ya nusu ya mlo kwa sababu ina sumu inayojulikana kama mimosine ambayo inasababisha kunyonyoka manyoya

2-Pia hutumika katika kuongeza mbolea kwenye udongo kwa kiasi cha N 2-45%, P 0.2-0.4%, K1.3-4%, Ca0.8-2% na Mg 0.4-1%, hupandwa kwenye shamba linalopumzishwa au kuchanganywa na mazao ili kurutubisha ardhi.

3-Kwenye maeneo yaliyoathirika na ukataji wa miti, leucaena hutumika katika kurudisha uoto. Hii ni kwasababu inakua haraka sana na inasambaa kama moto nyikani, inaweza kupandwa kwa kumwaga mbegu na zikaachwa kuota zenyewe au kwa kupanda miche. Kama kuna sehemu unataka ijae miti haraka panda miti hii hata kama ni michache itasambaa yenyewe, ingawa kwenye sehemu zenye baridi inakua kwa tabu kidogo.

4-Mbegu zake zinaweza kuliwa baada ya kukaangwa kama bisi, hii hufanyika mara nyingi wakati wa uhaba wa chakula kwa sababu ukusanyaji wa mbugu unasumbua kidogo

5-Matumizi mengine ni mbao, kuni na fito za kujengea, miti hii hutoa mbao nyekundu ambazo zinaweza kutumika kwa matumizi mbalimbali.

Saturday, September 29, 2007

FRIESIAN


ASILI YAKE
Uholanzi katika jimbo la frisieland
UZALISHAJI KWA MWAKA
10,158 kg za maziwa
3.64% mafuta
3.05% protini
RANGI
nyeupe na nyeusi, mara chache (1/1000) nyekundu na nyeupe
UZITO
kilo 1200 majike
kilo 1400 madume
Huyu ndiye aina ya ng'ombe anayeshikilia rekodi ya uzalishaji maziwa kwa kiwango cha juu, maziwa yake hayama mafuta mengi. Nimeshuhudia akitoa maziwa zaidi ya lita 70 kwa siku kwa mikamuo mitatu 1- lita 30 2- lita 20 3- lita 25. Madume yanatumika kwa kulimia na kukokota mikokoteni, Ni mkubwa kushinda nyati ambaye ana uzito wa kilo 800-1000, kama wanavyoonekana kwenye picha urefu wao ni sawa na kimo cha mtu mwenye urefu wa wastani. Kwa Tanzania wanapatikana zaidi Kitulo mkoani Iringa na Uyole (kilimo) Mkoani Mbeya

Thursday, September 27, 2007

KASUKU dondoo za kumfundisha kuongea

Mbegu kubwa ni waongeaji wazuri, mbegu ndogo ni wavivu kujifunza
Akiwa mdogo anajifunza vizuri zaidi, ukiweza mpate yule anayetoka kulelewa kwenye kiota
Kasuku muoga hawezi kujifunza vizuri.
Kasuku mwenye tabia ya kung'ata anauwezo mkubwa wa kujifunza kungea.
Kumbuka kasuku hujifunza maneno machache tu hawezi kuongea kama mtu.
Sehemu nzuri ya kumuweka nyumbani ni jikoni, kwa sababu kuna shughuli nyingi.
Huanza kuongea katika umri wa miezi 4-6.
Wakati wa kumfundisha zima radio na TV (kusiwe na kelele)
Muda mzuri wa mafunzo ni asubuhi na jioni.
Mfundishe kupiga miluzi baada ya kuweza kuongea baadhi ya maneno na si kabla ya hapo.
Kumbuka kasuku hujifunza vizuri zaidi kwa vitendo mfano unamtoa nje ya kibanda chake huku unamwambia " toka nje mmmh" ukirudia rudia, jitahidi kutumia Mmmh kila baada ya neno, hii humsaidia kujifunza kwa urahisi.
Hakikisha anapata mlo kamili maji na matibabu
MORE INFO rhxoqsa@hotmail.com

BASENJI


Moja ya mbegu ndogo za mbwa. Asili yake ni Afrika Mashariki, kumbukumbu zake zinapatikana kwenye ma piramidi ya kale kwa njia ya michoro
Ukienda vijijini utawakuta na ni maarufu sana kwa kazi ya uwindaji
Ni mbwa ambaye hana tabia ya kubwaka bwaka hovyo, wakimya makini, anajiamini
Jina la mbwa koko limetokana na mbwa huyu

Monday, September 24, 2007

KICHAA CHA MBWA


KUSAMBAA


Kichaa cha mbwa kinaweza kusambazwa na mate ya wanyama, wengi tumezoea kwamba mbwa ndiye anasambaza kichaa, lakini wanyama wengine kama paka, popo, ng'ombe, mbweha, fisi na wengine wanaweza kukisambaza




DALILI ZA MBWA MWENYE KICHAA


siku 1-3 mbwa hubadilika zile tabia ulizozizoea hapa ningumu kidogo kugundua


siku 3-4 mbwa huwa na aibu na pia huwa anakwepa mwanga, anajifichaficha na kung'ata kila kitu kinachopita karibu yake hata kama kimepeperushwa na upepo


siku 5 mbwa huanza kulemaa (paralysis) akianzia miguu ya nyuma kisha kufuatia ya mbele, baada ya siku saba mbwa hufariki
CHANJO
Mbwa wachanjwe dhidi ya kichaa angalau mara moja kwa mwaka, watoto wanaozaliwa na mama aliyechanjwa wachanjwe baada ya miezi mitatu baada ya kuzaliwa, unaweza kuwachanja kabla kama kuna mlipuko wa kichaa cha mbwa

Answers To Your Dog Care Questions!

VACCINATING YOUR NEW DOG
When puppies are born, their immune systems are not mature enough to make antibodies until approximately 8 to 12 weeks of age.

PARASITE CONTROL
Intestinal parasites are common in puppies. Puppies can become infected with parasites before they are born or later through their mother's milk.

HEARTWORMS
Heartworms are important parasites, especially in certain climates. They can live in your dog's heart and cause major damage to the heart and lungs.

YOUR DOG'S FOOD
UR DWhat to feed your dog, how much to feed and how often you feed are all vital questions to your dog's long term health.

CRATE TRAINING
Give your new friend a special place it may call his own. Your dog will use this place to rest and sleep, and it will feel safe and protected here. It must be cool and not a hot place, if you live in hot regions like Dar es salam, it must be built by using timber and not iron sheets

FOR MORE INFORMATION
rhxoqsa@hotmail.com

GREAT DANE

Hii ni moja ya mbegu kubwa za mbwa

HEIGHT
male 30-32 inches
bitches should not be less than 28 inches

COLOUR
yellow gold with a black mask,Black should appear on the eye rims and eyebrows, and may appear on the ears and tail tip. The deep yellow gold must always be given the preference. White markings at the chest and toes, black-fronted dirty colored fawns are not desirable

GAIT
The gait denotes strength and power

DISQUALIFICATION
Danes under minimum height.Split nose. Docked Tail.Any color other than those described under "Color, Markings and Patterns."

BULL DOG

SIZE
males 50 pounds
bitches 40 pounds

COLOUR
(1) red brindle, (2) all other brindles, (3) solid white, (4) solid red, fawn or fallow, (5) piebald, (6) inferior qualities of all the foregoing.


GAIT
a loose-jointed, shuffling, sidewise motion

DISQUALIFICATION
Brown or liver-colored nose.

DOBERMAN PINSCHER

HEIGHT

male 26-28 inches

bitches 24-26 inches

COLOUR

white, red & white patches on chest or legs

GAIT

free balancing, vigorous

GERMAN SHEPHERD


HEIGHT
males 24-26 inches
COLOUR
combination of black, brown & a little white
GAIT
a trotting dog
DISQUALIFICATIONS
Cropped or hanging ears.
Dogs with noses not predominantly black.
Undershot jaw.
Docked tail.
White dogs.
Any dog that attempts to bite the judge

USINGIZI WANGU


Hapo ni fox na tobby