Monday, September 24, 2007

KICHAA CHA MBWA


KUSAMBAA


Kichaa cha mbwa kinaweza kusambazwa na mate ya wanyama, wengi tumezoea kwamba mbwa ndiye anasambaza kichaa, lakini wanyama wengine kama paka, popo, ng'ombe, mbweha, fisi na wengine wanaweza kukisambaza




DALILI ZA MBWA MWENYE KICHAA


siku 1-3 mbwa hubadilika zile tabia ulizozizoea hapa ningumu kidogo kugundua


siku 3-4 mbwa huwa na aibu na pia huwa anakwepa mwanga, anajifichaficha na kung'ata kila kitu kinachopita karibu yake hata kama kimepeperushwa na upepo


siku 5 mbwa huanza kulemaa (paralysis) akianzia miguu ya nyuma kisha kufuatia ya mbele, baada ya siku saba mbwa hufariki
CHANJO
Mbwa wachanjwe dhidi ya kichaa angalau mara moja kwa mwaka, watoto wanaozaliwa na mama aliyechanjwa wachanjwe baada ya miezi mitatu baada ya kuzaliwa, unaweza kuwachanja kabla kama kuna mlipuko wa kichaa cha mbwa

No comments: